Zusammenfassung der Episode
Katika mkutano wa tabia nchi mwaka huu COP31, jijini Antalya, Uturuki, wadau mbalimbali wamesisitiza dunia kuondoka katika kutoa ahadi na kuanza kuleta matokeo ya haraka na yenye tija. Sayari imekuwa ikikabiliwa na changamoto kubwa za mabadiliko ya tabianchi, mkutano wa mwaka huu unalenga zaidi kuharakisha mabadiliko ya nishati safi na kusukuma vitendo madhubuti vya kimataifa. Nchi zimesisitiza kuwa muda wa mijadala umekwisha na ni muda sasa wa utekelezaji wa vitendo. Nimefanya uchambuzi na Cherop Soy kutoka shirika la Enzi Ijayo, akizungumzia masuala ya nishati safi kama vile matumizi ya magari ya umeme.
Katika mkutano wa tabia nchi mwaka huu COP31, jijini Antalya, Uturuki, wadau mbalimbali wamesisitiza dunia kuondoka katika kutoa ahadi na kuanza kuleta matokeo ya haraka na yenye tija. Sayari imekuwa ikikabiliwa na changamoto kubwa za mabadiliko ya tabianchi, mkutano wa mwaka huu unalenga zaidi kuharakisha mabadiliko ya nishati safi na kusukuma vitendo madhubuti vya kimataifa. Nchi zimesisitiza kuwa muda wa mijadala umekwisha na ni muda sasa wa utekelezaji wa vitendo. Nimefanya uchambuzi na Cherop Soy kutoka shirika la Enzi Ijayo, akizungumzia masuala ya nishati safi kama vile matumizi ya magari ya umeme.
Folgen
Ajenda ya Nishati Safi na Vitendo Badala ya Maneno Zatawala Mazungumzo ya COP31 Uturuki
GehörtKatika mkutano wa tabia nchi mwaka huu COP31, jijini Antalya, Uturuki, wadau mbalimbali wamesisitiza dunia kuondoka katika kutoa ahadi na kuanza kuleta matokeo ya haraka na yenye tija. Sayari imekuwa ikikabiliwa na changamoto kubwa za mabadiliko ya tabianchi, mkutano wa mwaka huu unalenga zaidi kuharakisha mabadiliko ya nishati safi na kusukuma vitendo madhubuti vya kimataifa. Nchi zimesisitiza kuwa muda wa mijadala umekwisha na ni muda sasa wa utekelezaji wa vitendo. Nimefanya uchambuzi na Cherop Soy kutoka shirika la Enzi Ijayo, akizungumzia masuala ya nishati safi kama vile matumizi ya magari ya umeme.
Mkutano wa COP17: Hatua Mpya Zazinduliwa Kuokoa Viumbe Hai Duniani kule Armenia
GehörtWakati ulimwengu ukiwa katika njia panda kutokana na kasi ya kupotea kwa viumbe hai na mabadiliko ya tabianchi, mji mkuu wa Armenia, Yerevan, kuanzia Oktoba 19-30 mwaka huu ulikuwa kitovu cha matumaini mapya. Kupitia mkutano wa Umoja wa Mataifa wa bayoanuai wa COP17, viongozi wa kimataifa, wanasayansi, na wanaharakati wamekutana sio tu kujadili changamoto zinazokabili sayari yetu, bali kuweka Ahadi ya Yerevan, mpango ambao unalenga kugeuza maneno kuwa vitendo ili kulinda utajiri wa asili wa dunia yetu kwa vizazi vijavyo. Katika makala haya nimezungumza na Stephen Basele, mkurugenzi wa wakfu wa malengo ya wafugaji, kaskazini mwa Kenya aliyehudhuria mkutano huu kutetea haki za jamii asilia.
Awamu ya pili: Kongamano la masoko ya kaboni barani Afrika, Kigali
GehörtPamoja na Bwana Zephaniah Kivungi, mkurugenzi wa tabianchi katika shirika la CIFF, tunaendelea na awamu ya pili ambapo nilikuahidi kuangazia ni kwa namna gani tunaweza kuhakikisha kuwa biashara ya kaboni zinawakilisha upunguzaji halisi wa gesi chafuzi.
Afrika: Nini nafasi ya masoko ya kaboni katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi
GehörtMasoko ya kaboni, yapo kwa ajili ya kuwawajibisha watu na mashirika ambayo shughuli zao zinachangia katika uchafuzi wa hewa, ambapo wanahitajika kugharamia juhudi zinazofanywa na watu mbalimbali au jamii katika kupunguza hewa ya kaboni kwenye anga, kwa mfano upandani wa miti. Nimemwalika, Zephaniah Kivungi, mkurugenzi wa tabianchi katika shirika la CIFF, ambaye atatusaidia kuelewa zaidi suala hili la masoko ya kaboni katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.
Kenya: Sahihi Elfu sitini za kuitaka serikali kusitisha ukataji wa miti kwenye misitu ya umma
GehörtMadai ya wanaharakati pia yanaitaka serikali kusitisha mipango yoyote ya kutenga maeneo ya misitu kwa ajili ya matumizi mengine, kama vile ujenzi wa barabara, kudumisha marufuku ya ukataji miti ili kulinda misitu iliosalia nchini Kenya, na kuchukua hatua za haraka na thabiti dhidi ya shughuli za ukataji miti kinyume cha sheria na uporaji wa ardhi ndani ya maeneo ya misitu